Ninayo furaha kubwa ya kua mbele yenu siku ya leo. Nimelazimika kuchukua mzigo huu mkubwa kabisa wa kuongoza Emo ‘ya M’mbondo hapa Perth . Kama mwana member wa Emo ni haki yangu ya msingi kuchagua au kuchaguliwa. Hivo basi, nazani kwa ushurikiano wenu, wote tutaweza kufanya Emo ‘Ya M’mbo Perth kuwa Jamii moja, imara na yenye maendeleo .
Hii ni zamiri yangu tu. Ila watakao lifanikisha hili ni nyinyi. Tunaweza kufikia hapo kwa kubadili tabia zetu ambazo mizizi yake imejikita kwenye mambo madogo madogo kama vile: misiba, kujifungua kina mama wajawazito, harusi ao tafrija.Hapa namaanisha “ malanda o bonga male malya”.
Kwa sasa lengo la uongozi wetu ni mshikamano ,mipango na maendeleo. Tujiulize Emo ‘ya M’mondo ilianza lini duniani? Nani alianza Emo ‘Ya M’mbondo duniani? Iko wapi? Emo iliisha fanya nini kwa Wabembe Duniani ,Australia ,Perth, Congo, au Fizi?
Jibu ya maswali yote hayo ni kwamba, Emo ‘Ya M’mbondo ina historia kubwa. Ilianza tangu kuzaliwa koo za M’bembe wa Kwanza na kililenga maendeleo yao. Ila ,hadi sasa maendeleo wabembe ni machahche sana duniani ukilinganisha na makabila mengine ambayo ni jirani zetu.
Utofauti wetu ni upi? Ukweli ni kwamba Wabembe tumeshindwa kupanga miradi ya maendeleo. Ama tukipanga , hatuendelei. Tunayo mifano mingi sana: SOCODEFI, ACCOREFI, ASMAKU, BDC/Mshimbakye, bila kusaau kanisa la Methodist Libre. Ukweli ni kwamba mipango bila mshikamano hakuna maendeleo. Je , leo tunaitaji kupanga kama wale waliotutangulia? Wapi walipo kosea ili tusikosee na sisi ? Ukweli ni kwamba “kushindwa kupanga ni kupanga kushindwa” ,kama tunavyo sema kwenye Kibembe kwamba “Mbama ya lúkendo ekyo lala ya lúngwa”. Leo natamani kuwaambia mipango yetu.
1. Mwaka huu kutakuepo na vikao vya baraza kuu vitatu (Mwezi huu, mwezi wa sita au juna pia mwezi wa saba). Lengo nikuchukua maamuzi muimu ya Emo.
2. Pia tutakua na ziara mbalimbali kwenye ma offisi ili tupate fursa ya kukitangaza Emo kwa wafazili, waisani na wawekezaji mbali mbali.
3. Tutakua na seminar mwezi wa saba . Lengo la seminar hii nikufaamishana mila na desturi za kibembe, maendeleo ya kibembe na wabembe sehemu mbali mbali . Tutapata fursa ya kuwaita wabembe wa maeneo mbalimbali ili waje tubadilishane uzowefu na kujua kile ambacho tunatakiwa kufanya katika ulimwengu huu wa utanda wazi ambao kizazi cha kwanza cha M’mbondo akikupata bahati yakuona.
4. Tutakua pia na sherehe za kumbukumbu ya Mauwaji ya makobola ilio fanyika tarehe 29 -31 /Dec.1998. Hii fursa tutaitumia kufaamisha ulimwengu mzima kilichotufanya tuache maskani yetu nakuweza kujikuta hapa Australia.
5. Hatutaishia hapo tu, tuna lengo la kukusanya Dollar 10,000 (elfu kumi) mwaka huu ili tuweze kuwa na miradi mbali mbali ya maendeleo kama vile Shop na Centre Culturel ya Wabembe.
6. Tutakua pia na maswala mbalimbali ya Jamii: Kina mama, vijana, wazee. Tutaweza kutembelea kina mama walio jifungua na watu wenye matatizo mbalimbali.
7. Uchaguzi wakamati mpya itakuepo mwezi wa kumi na mbili.
Ndugu zangu,
Kazi hii ni kubwa sana kama mutaikubali. Inaitaji msaada wenu. Msaada wa hali na mali kufanikisha hili. Naomba kamati kuu irizie mabadiliko yafuatayo kwenye katiba:
1. Sheria ya mapato na usimamizi wa fedha: Kila mwana member atakaye shindwa kutowa mchango wake wa iyari ,achukuliwe hatua za kinizamu kama kusimamishwa uwana chama wake na kunyimwa haki za uwana chama kama kuchagua na kuchaguliwa .
2. Sheria ya Matumizi ya Chama: Tunapo jikuta kwenye bank tuko na dollar 3,000 bila kujua tufanye nazo nini ndo hapo tuna nunua kile ambacho hatuitaji. Tunavitu kwenye Emo , ambavyo si vya lazima au havitumiki : Guitars, Keyboard ,etc. Hivi vitu ni lazma tuvifanyie kazi. Ivyo basi, tunaomba Watendaji wa chama wawezeshwe ili kazi yao iwe yenye kukamilika: usafiri na mawasiliano.
3. Malipo au Michango ifanyike directly kwenye Account ili kupunguza usumbufu.
4. Kila mwisho wa mwaka , members wapewe Certificates of donation ili wapate ku claim donation tax rebate.
5. Emo iwe na Muhuri wake kama Chama.
Ndugu zangu,
Mambo mengine yanaweza jitokeza hapo baadaye. Mabadiliko tutakabiliana nayo. Nawakilisha hoja Kamati kwenu kama Baraza kuu ili muweze kujadili .Túle bani ,tuikange ifumba.
Asante.
Maitre Philbert Bilombele, A. (MIR)
Katibu Mtendaji.
Habari zenu
ReplyDeleteMimi mi mbembe nipo Tanzania kwa hakika nimefurahishwa na hatua mnazochukua baada ya kufika huko nchi za watu